Leo tarehe 17 Aprili, 2024, Taasisi ya Rugambwa Girls Foundation kwa kushirikiana na baadhi ya Wanafunzi waliosoma shule ya Sekondari Rugambwa ambao siyo Wanachama wametoa msaada wa mahitaji mbali mbali yenye thamani ya TZS. 3,260,000.00 kwa mabinti 52 wanaosoma shuleni Rugambwa walio na uhitaji. Malengo ya TAASISI hii ni kuhakikisha mabinti wanasoma bila changamoto zinazoweza kuwafanya wasisome vizuri na kujiingiza katika tabia hatarishi
Ndugu Georgia George akisoma RISALA ya kukabidhi msaada uliotolewa na Rugambwa Girls Foundation.
Baadhi ya Wanafunzi waliopokea msaada wa vitu mbali mbali kutoka Rugambwa Girls Foundation
Kwa kushirikiana na Mkuu wa Shule ya Rugambwa Sekondari, Taasisi ilipata orodha ya mahitaji muhimu kwa Wanafunzi hao ambao baadhi yao ni walemavu na pia wanatoka kwenye familia duni. Kila mara Taasisi ya Rugambwa Foundation inawasiliana na Mkuu wa Shule kuona mabinti wana changamoto zipi na kuwajulisha Wanachama ambao huchangia kile wanachojaliwa kusaidia ili kupunguza changamoto hizi.
Baadhi ya Wanafunzi waliopokea msaada wa vitu mbali mbali kutoka Rugambwa Girls Foundation
Taasisi inawaalika akina MAMA wote waliosoma katika Shule ya Sekondari Rugambwa kujiunga na Taasisi ili kwa pamoja tuunganishe nguvu zetu kuwasaidia mabinti wasome bila changamoto.
0 comments :
Post a Comment