Rugambwa Girls Foundation ilifanya Mkutano wake Mkuu tarehe 22 Oktoba, 2022, Morogoro. Katika Mkutano huo, wajumbe walitoka sehemu mbalimbali za nchi ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.
Mkutano uliweza kupokea mapendekezo ya namna ya kuboresha uendeshaji wa RGF. Vilevile Mkutano uliweza kupokea taarifa ya msaada uliotolewa shuleni kusaidia shule kuvuna maji, uliopokelewa shuleni na RAS Kagera.
Vilevile Mkutano uliweza kupokea taarifa ya kujiunga na Bima ya Nishike Mkono na uwekezaji katika UTT.
Mkutano huu, pia ulishuhudia kufanyika kwa uchaguzi wa Viongozi wapya na waliomaliza muda wao walishukuliwa na kupewa mkono wa asante.
Na wajumbe walijadili mpango mkakati na mpango kazi kwa kipindi kijacho.
0 comments :
Post a Comment