Kutoka kushoto ni Dr. Siima Bakengesa (KATIBU RGF), Prof. Faustine Kamuzora (KATIBU TAWALA MKOA), Bi. Kagemulo (Mkuu wa Shule ya Rugambwa) na Bi. Kazimoto (Mwakilishi wa Afisa Elimu Mkoa).
Tarehe 26 Julai, 2021, Taasisi ya Rugambwa Girls
Foundation ilikabidhi SIM TANK (Matenki) tano (5) za kuhifadhi maji. Kati ya hizo tatu (3) ni za lita 5,000 na
mbili (2) ni za lita 10,000 jumla lita 35,000 pamoja na vifaa vya kuvunia maji
ya mvua (Gutters) katika shule ya Sekondari Rugambwa iliyoko Mkoani Kagera.
Hii ni katika Kuunga juhudi za kumsaidia mtoto wa Kike katika elimu yake kwa kuondoa kikwazo cha uhakika wa upatikanaji wa maji kwa kuvuna maji ya mvua.
Msaada huo uliwasilishwa na Dr. Siima Bakengesa ambaye ni KATIBU wa Taasisi ya Rugambwa Girls Foundation na ulipokelewa na Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Rugambwa.
0 comments :
Post a Comment