Leo tarehe 3 Juni, 2020 Taasisi ya Rugambwa Girls
Foundation (RGF) imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco E.
Gaguti msaada wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa (COVID 19) unaosababishwa na
virusi vya Corona vyenye thamani ya TZS. 2,000,000/= kwa Wanafunzi na Walimu wa
shule ya Wasichana ya Rugambwa Sekondari iliyoko Wilaya ya Bukoba Mjini,
Mkoani Kagera ikiwa ni Kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais wetu pamoja na Serikali
aliyeruhusu shule kufunguliwa kwa kidato cha sita na kuungana na wazazi,
walimu, walezi na wanajumuiya wa Rugambwa na wanafunzi wa kidato cha sita kuunga juhudi za elimu kwa mtoto wa Kike.
Mwakilishi wa Taasisi
ya Rugambwa Girls Foundation, Bi. Beatrice Van Arkadie akikabidhi msaada wa vifaa
vya kujikinga na ugonjwa wa COVID -19 unaosababishwa na virusi vya Corona kwa
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti
Afisa
Elimu, Mkuu wa Shule, Mkurugenzi wa Mkoa, Mkuu wa Mkoa na Mwakilishi wa Rugambwa Girls Foundation,
wakiwa kwenye Picha ya Pamoja
Rugambwa
Girls Foundation (RGF) imesajiliwa Novemba 2015, kwa namba ya usajili na 5216 kwa sheria Cap 318 R.E 2002. RGF
inaundwa na wahitimu wa Rugambwa
Sekondari., hadi sasa Foundation hii ina wanachama 40 walioko katika mikoa
mbalimbali ya Tanzania. Jumuiya yetu
haizalishi faida (non profit organization)
Lengo kuu la RGF ni
kusaidia mtoto wa kike kujitambua
na kupambana na changamoto mbalimbali za elimu. Pamoja na hayo, RGF pia inajihusisha na sekta ya Afya,
Mazingira na Ujasiliamali. Pamoja na kusaidia jamii kwa kutumia fedha
tunazojichangisha, pia tunasaidiana wenyewe kwa wenyewe katika ugonjwa,
sherehe, misiba na majanga mbalimbali, kwa kutumia miongozo tuliyojiwekea. RGF Tuna
malengo ya muda mrefu na muda mfupi, ikiwamo kuanzisha Benki, kujenga mabweni,
na kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum shuleni Rugambwa, na kuwapa huduma.
Miaka ya Nyuma kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi,
Mkoa wa Kagera tuliweza kufanya kampeni
ya kuhamasisha wanafunzi wa Rugambwa juu ya kujitambua. Mikutano miwili
ilifanyika shuleni Rugambwa na vilevile tumeweza kuwasaidia wanafunzi
wasiojiweza na wenye ulemavu mbalimbali. Wenye uoni na usikivu hafifu na wenye ualibino kwa kuwapatia bima za afya na mahitaji kama
vile madaftari, kalamu, taulo za kike na mafuta ya ngozi kazi ambayo
inaendelea. Vilevile na tulifanya harambee kuchangisha fedha za
kuweza kuinua miundo mbinu ya Rugambwa Sekondari ambapo kwa kushirikiana na TEA
na wadau mbalimbali tulikusanya jumla ya Shilingi milioni 129 ambazo zimetumika
kukarabati miundo mbinu hapa shuleni na kuboresha miundo mbinu ya walemavu..
Msukumo huu pia ulitoka shuleni ambapo walituomba tuweze kusaidia pale
tunapoweza. Tunaamini juhudi hizi zimepelekea matokeo ya Rugambwa kuwa mazuri.
0 comments :
Post a Comment