Mwanachama wa Rugambwa Girls Foundation Bi. Judith Rushanja Ndissi
atoa msaada wa kumlipia Bima ya Afya ya mwaka mzima mtoto Maimuna Yahaya Mamisu mwenye ulemavu aliyeongozana na Mama yake Bi. Tunu Juma Maziku mkazi wa
Tanga ili aweze kuendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Bi. Ritha Kamala akikabidhi
msaada kwa Bi. Tunu Juma Maziku kwa ajili ya mwanae Maimuna (kwenye
picha)
Uongozi wa Rugambwa Girls Foundation uliletewa taarifa ya uhitaji wa
Bima ya afya kwa mtoto Maimuna Yahaya Mamisu kupitia kwa mwanachama mwenzetu Ritha
Kamala ambaye alikutana na Bi. Tunu Juma Maziku akiwa na mwanae Maimuna wakiwa
kwenye mizunguko ya kuomba msaada kwa wananchi ili wapate hela hiyo na ndipo
alipoutaarifu uongozi na Mwanachama mwenzetu Judith Rushanja Ndissi alijitolea na
kumlipia Maimuna, Bima ya Afya ya mwaka mzima.
Bi. Judith Rushanja Ndissi
aliyetoa msaada wa Bima ya Afya ya mwaka mzima kwa mtoto Maimuna (kwenye picha)
Uongozi unatoa wito kwa Wanachama wote wa RGF kujitolea katika kutoa
misaada kwa wahitaji.
Asante sana Mama Ndiss kwa msaada wako. Mwenyezi Mungu akubariki sana.
ReplyDeleteAsante sana Mama Ndiss kwa msaada wako. Mwenyezi Mungu akubariki sana.
ReplyDelete