Mkutano
Mkuu wa Tatu (3) wa Rugambwa Girls Foundation uliofanyika katika ukumbi wa
Defrance Hotel, Sinza, Dar es Salaam, ulipitia maazimio yaliyowekwa kwenye
Mkutano Mkuu wa pili (2) uliofanyika tarehe 18 Februari 2017 katika ukumbi wa
Hotel Defrance, Sinza, Dar es Salaam na kujadili utekelezaji wa maaziimio hayo.
Na
pia Mkutano Mkuu ulijadili zaidi jinsi ya kuinua elimu shuleni Rugambwa, na
jinsi ya kupata pesa za kuweza kukarabati baadhi ya miundo mbinu ya shule,
vilevile Mkutano ulijadili jinsi ya
kutafuta mahusiano na taasisi nyingine ambazo zinaweza kutoa msaada kwenye
shule hiyo.
Pia
Mkutano huu umesisitiza zaidi kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji
maalum (kwa walemavu wa aina zote) na kuendelea kuwalipia Bima ya afya
wanafunzi 21 ambao pia walikuwa wamelipiwa awali.
Mkutano
uliwakaribisha wanachama wapya na kuchagua viongozi wapya watakao ongoza umoja
huu kwa muda wa miaka mitatu ijayo.
0 comments :
Post a Comment