Mgeni Rasmi (Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh. Jackson Msomi) akikabidhi msaada kwa watoto wenye ulemavu
Taasisi ya Rugambwa (Rugambwa Girls Foundation) inayoundwa na baadhi ya wanafunzi wahitimu wa shule ya Sekondari ya Wasichana Rugambwa tumetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya kila siku kwa wanafunzi wenye ulemavu wa aina mbalimbali wanaosoma katika shule ya Sekondari Rugambwa, vitu vilivyo tolewa ni Kalamu, sabuni, dawa za meno, mafuta ya kujipaka, lotion maalum wa ajili ya wenye ulemavu wa ngozi na taulo za kujihifadhi wakati wa hedhi (PAD). Pia jumla ya wanafunzi 21 wenye mahitaji maalumu wamelipiwa huduma ya Bima ya Afya (NHIF) kwa kipindi chote watakacho kuwa shuleni hapo.
Wanafunzi walio lipiwa Bima ya Afya ni wenye ulemavu wa Viungo, upofu wa macho, viziwi na walemavu wa ngozi.
Mgeni Rasmi katika hafla hii alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mheshimiwa Jackson Msomi.
Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu
Baadhi ya wanafunzi wa zamani waliohitimu shuleni Rugambwa (Kutoka kushoto ni Kagemulo Lupanga Mkuu wa shule, Janeveva Lugumamu, Tiliphina Bachwaki na Nyesige Mtembei)
Bi Janeveva Lugumamu akiwa katika picha na baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu
Kushoto ni Nyesige Mtembei na kulia ni Georgia George wahitimu wa zamani shule ya Sekondari Rugambwa
Kushoto ni Agripina Kalabamu na kulia Janeveva Lugumamu wahitimu wa zamani
Wanahabari kazini
Vipaji katika kucheza
Pia wanafunzi walipata soda
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Rugambwa akiongea
0 comments :
Post a Comment